Sunday, October 28, 2018

Re: NDOA YA MAMA

On Oct 29, 2018 00:11, "Brighton Sanga's" <sangasb46@gmail.com


>
>

                   NDOA ƳA MAMA
  
       Alitoka mwanamama aliye onekana ni mwenye sura iliyotawaliwa na alama za viulizo? Na umri waƙe usiopungua miaka ishirini na kenda,
> kwa makadirio ya urefu kama futi tano  niliweza kumtambua kwa haraka  kuwa ni mwnyeji wa ardhi ile ile inayosifika kwa mahaba yenye ghaiba na upendo maridhawa duniani, kote tangu na kabla hatujajua ni lini angepelekwa kwa malkia na kurudishwa mjini kisha tugende ziwani kwa tanzia mawimboni.
>
>          lakini mwembamba na mwenye rangi ya  jongoo asiyejikunja mviringo, akiwa amevalia vazi la khanga na blauzi aliyo tunzwa siku  za  maandalizi ya ndoa yake, viungo vyake vya mafikiro vilionekana dhaifu kwa msongo wa mawazo wa sokomoko zisizo kwisha kila uchwao za dhulma ya mapendo na huduma ya vilindi apatayo kila baadaya masika tano kipimdi cha maandalizi ya ndoa yake.
>
>        Marika  huƴu haƙuoneƙana ni mwenye mafanikio na ndoa  yake iliyofungwa kwa ahadi ambazo hazija tekelezwa mpaka sasa. Nguo mpya  alizotunzwa kwenye maandalizi ya ndoa yake zilikuwa zimeshatatuka tatuka  tayari kwani zinapata masika tatu sasa tangu atunzwe. Na mwenyewe akiwa dhofulghali  yu taabani..... anashusha beseni la nyanya kilemɓa ƙina dondoƙa kichwani mtindo wa twende kilioni zilizo fumuka na kushikamana na magodoro. Anafungua khagha alio funga butu kifuani mwake, anamtua mtoto. Anainamia kwenye khanga ilio napicha ya mtu na maneno ya ahadi ya ukombozi wa ndoa yaƙe anafuta! ili mtoto wake asigundue kama analia...! Anagugumia anaongea kwasauti ya chini... Huku aki fvyonza fvyonza  kamasi zisitiririke kwenye paji la uso akaongea kwa uchungu....
>
>       walikuja wawili wakwanza alifika mapaƙa nyumɓani kwa saɓaɓu alikuwa maarufu na mwenƴe maneno mengi na mwingi wa ahadi na ƙilicho mpa uwaminifu ni kwakuwa ana watu wengi wenye wa sifu, ɓasi kwavile nilikuwa ni mbichi wa kuvunja ungo na aƙili za kushikiwa na wazazi nilipo tunzwa tu doti ya khanga, kofia na pesa kidogo ndipo imani ilipozidi akanipa ahadi ya elimu, ajira kwa shemeji zake wa ɓoda ɓoda, miƙopo kwa wote dume huyu aliongea haya mbele ya kadamnasi mapaƙa nilishindwa kukataa nilipolinganisha na mausia ƴa mama.
>
>        Yule wa alinitafuta kwa muda wake huku akininong'oneza anaƙudanganƴa huyo laƙini hauonekana kuwa na uwa na nguvu kwa saɓaɓu alishindwa hata kuonana na wazazi wangu ila alifanikiwa kuwachukuwa kaka zangu ili wa weze kuniƙomɓoa mimi ila walishindwa kwa kuwa kila wanapoweka mijadala huwa awafikii lengo wanaaribiwa na bwana wa kwanza.
>
>      Mwezi wa toɓa ulipowadia ndoa yangu ilifungwa na dunia yote ilindirima kuolewa kwangu leo hii namlaumu mzazi wangu kwa kuniruɓuni kunichagulia asiye chaguo langu bwana mkatili,muongo,nafiki, asiye na mapenzi hata kwa vimzake, nyumɓani haonekani yeye anaishi kilingeni kule kwenƴe vigoda vƴa mzunguko amesahau ƙama ameacha mwali aliƴe muongopea kwa ahadi kedekede
>
> MUACHE MTOTO ACHAGUE ATAKACHO
>
>                Mtunzi : brighton sanga
>                         0718 727204
>      
>         
>      

Saturday, October 27, 2018

MASHAKA YA SAA MBOVU

MASHAKA YA SAA MBOVU

Upepe mkali ulivuma, ulio ambatana pamoja na ngurumo vumbi kali jeusi lilitimka timu timuu.. Miti mikubwa pamoja na minazi iliyo pepesuka mithili ya gari bovu kwenye mlima wa changarawe!


Baadaya mbilingembilinge zote hizi kutokea kulionekana wakazi wa pale waki pita pita maeneo tofauti tofauti kwa shughuli zao za hapa na pale,

Mwali mbichi mwembamba rangi ya maji ya chungwa, sura ya duara na macho mviringo wa yai ya kulegea kama aliyekula kungu, chuchu za saa sita na nyonga zinazoendelea kukua kwa kasi urefu wa futi 5 na umri wa miaka 19. Jina lake BETINA.

BETINA iliokota saa iliyo onekana siyo mpya ambayo hakutarajia kuipata kwani ilonekana ikale kidogo iliyo mpita kama masika kumi, iliyo valia kwa mtindo wakisasa haswa tena wa kijana leo! Ni saa iliyo mfurahisha mlibwende huyo na wengine wote walio mzunguka katika nƴakatizake zote kwa sababu yeye ni saa!

Saa ya BETINA ili msaidia sana wakati wote alipo ihitaji kuitumia ilienda sawa na kumfurahisha binti huyu pasi na sokomoko! Na hadithi rejea wala ngonjera ya aina yoyote ile aliamini saa hii na kutajiwa muda wowote pindi anapoiuliza!

Saa ilipoanza kupoteza nyakati usiku kusoma mchana na mchana kusoma usiku basi? mwali huvyu ili nyong'onyezwa sana kwa kuwa hakuzoea vitibwi! nadhurububa ya mahaba yaliyo kosa ghaiba yenyenyingi nasaba kwenye viwanja vyote vya sabasaba laaah mlibwende huyu hakujua kama kusamehe ni mara saɓa sabini na kusahau kuwa tafsiri ya kusahau ni kupuuza! nasio kulipiza kisasi au kukumbuka, Betina alipatwa na ngonjwa kubwa!

Ni mwenye kupoteza kumbukumbu, kuongea akiwa peke yake, mwenyekupenda ugomvi, kujiona hanathamani, kuto kujiheshimu basi familia iliendelea kuumizwa kichwa na binti yale wali tumia dawa za hospital mpaka kwa kalmanzila lakini hali iliendelea kua mbaya tena mbaya zaidi betina amepata kichaa kwa sababu aliathirika kwenye moyo na ubongo kwa ngojwa la SONONO.

Nigonjwa linalo athiri moyo na ubongo kupoteza kumbumbu,kujichukia,kuona unaonewa, kudhulumiwa, kujilaumu na kufanya mambo ambayo ujatarajiwa kuyafanya katika mazingira unayo ishi.


Ɓrighton sanga